ujauzito ni nini?
hii ni hali ya kiumbe{featus}, kimoja au zaidi kukua ndani ya kizazi cha mwanamke kwa kipindi maalumu. kipindi hiki hua ni wiki 37-42
vifuatavyo ni vitu muhimu vya kuzingatia kipindi hicho muhimu kwa matokeo mazuri ya mama na mtoto...
- mlo kamili i.e huu ni mlo unaochanganya vyakula vya aina zote kama protini, wanga, mafuta, matunda na mboga za majani, kila kirutubisho kikiliwa kwa kiasi kidogo kuupa mwili virutubisho vyote na kukwepa unene uliopitiliza ambao ni hatari sana kwa kipindi hiki.
- epuka unywaji wa pombe aina yeyote na uvutaji wa sigara i.e kemikali nyingi ambazo sio rafiki wa binadamu zinapatikana kwenye vitu hivyo, kwa hyo utumiaji wa vitu hivyo kipindi cha ujauzito huweza kusababisha kupanda kwa presha kipindi hicho, kutoka kwa mimba, kuzaliwa mtoto mwenye uzito mdogo na mwenye uwezo mdogo darasani na mengine mengi.
- usitumie dawa yeyote ambayo haijaandikwa na daktari i.e dawa nyingi zina madhara makubwa sana kwa mtoto hasahasa miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito, hivyo ni vizuri kumuona daktari mda wowote unapopata tatizo lolote. watoto wengi wanozaliwa miaka hii wakiwa na matatizo ya kutokua na viungo kadhaa vya mwili au maumbile tofauti ya kibinadamu husababishwa na utumiaji huu wa dawa bila mpangilio.
- ongeza ulaji wa folic acid i.e haya ni madini yanayopatikana sana kwenye mboga za majani na pia kuna vidonge muhimu vyenye madini hayo kutoka viwandani. utumiaji wake kabla na baada ya ujauzito husaidia kuzuia matatizo ya mfumo wa fahamu wa mtoto. mfano spinal bifida..
- ifahamu siku yako ya matarajio i.e hii ni ile siku yako ambayo unatarajia kujifungua. ukiifahamu itakuasaidia kujiandaa kifedha, kijamii na kisaikolojia kupokea mtoto mpya ndani ya familia na itakusaidia kuwahi hospitali pale ambapo mimba itakua imepitiliza mda wake wa kawaida. hesabu za hii za hii siku inapatikana kirahisi clinic ya baba mama na mtoto ambayo ni muhimu kuhudhuria mara tu unapopata ujauzito. kama hukumbuki siku yako ya mwisho kuona siku zako, kipimo cha utrasound scan kipatikanacho hospitalini bila madhara yeyote kinaweza kukusaidia.
kwa maelezo zaidi bofya hayo maneno ya kijani chini kusoma..
SECRETS OF GOOD HEALTH
NAKUTAKIA AFYA BORA WEWE NA FAMILIA YAKO.
MAWASILIANO 0653095635/0769846183
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
msaada wa elimu kuhusu chunusi ufanyike kupitia kwawa taalamu
JibuFuta