data:post.body Agosti 2014 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HIZI NDIO SABABU ZINAZOFANYA WATU WENGI HAWAPONI KABISA MADONDA YA TUMBO.{PEPTIC ULCERS]



Madonda ya tumbo ni nini?
Haya ni madonda yanayoshambulia tumbo la chakula{stomach} na utumbo mdogo {douedunum}.

chanzo ni nini?
Sababu kuu mbili muhimu zimegundulika ndio chanzo kikuu cha madonda ya tumbo kwa binadamu nazo ni.

Helocobactor Pylori: hawa ni bacteria ambao ni chanzo kikubwa cha ugonjwa huu na asilimia kubwa ya wagonjwa wamekutwa na bacteria hao wanapoenda kupimwa.

Non steroidal antiflamatory drugs: hichi ni kikundi cha dawa za maumivu ambazo kitaalamu zinafanya kazi kwa kuondoa hormone iitwayo kitaalamu kama prostiglandins ambayo  ni muhimu kwa kutunza tumbo lisipate madhara.  mfano diclofenac, ibuprofen, peroxicam, meloxicam na etc

Sababu zingine ni:
Uvutaji wa sigara: utafiti umeonyesha asilimia kubwa ya watu waliokutwa na ugonjwa huu walijuhusisha na uvutaji wa sigara lakini haifahamiki ni jinsi gani sigara inaleta mdonda haya.

Mgandamizo wa mawazo: mtu anapokua na mawazo sana{stress}, mwili hutengeneza hormone inayoitwa kitaalamu kama adrenaline ambayo hukunja mishipa mikubwa na midogo ya damu{vasoconstriction of arteries and arterioles} ya mwili mzima.
Mishipa hiyo ambayo na tumboni ipo, inapojikunja husababisha vidonda{ulcer}.
Kwasababu ya kukosekana damu ya kutosha kwenye seli za tumboni.

Genetics: baadhi ya koo zimeonyesha kurithi ugonjwa huu na japokua haijathibitika mahusiano yake yakoje.

               Dalili za madonda yalioko tumboni.{gastric ulcers}
    • Kichefuchefu na kupungua uzito kwani aina hii ya madonda ya tumbo humfanya mtu aogope chakula.
    • Maumivu makali wakati wa kula kwasababu chakula huingia tumboni na kuanzisha maumivu hapo hapo.
    • Kujisaidia choo nyeusi ni dalili kwamba madonda yanavuja damu.{digested blood is always black}                                                                                                                                                               dalili za madonda ya kwenye utumbo mdogo. 
    • Maumivu makali masaa matatu mapaka manne baada ya kula.
    • Kuongezeka uzito kwani maumivu ya aina hii ya madonda humfanya mtu ale sana ili kupata nafuu.
    • Kutoa choo nyeusi.

    Vipimo vya kugundua  madonda ya tumbo hospitalini:Bariaum meal na barium swallow:
    Hichi ni kipimo ambacho mgonjwa anapewa aina flani ya kimiminika na kunywa kisha picha ya x ray hupigwa kufuatisha kile kimiminika kuangalia kama kuna sehemu ina shape ambayo si ya kawaida tumboni.

    Esophagogastroduodenoscopy:
     hichi ni kipimo ambacho aina flani ya mpira ambao una camera kwa mbele,  hupitishwa  mpaka tumboni na kuonyesha picha ya tumbo kwenye screen kuangalia kama kuna tatizo lolote.

    Ultrasound scan:
    Kipimo hichi hutumia mashine ambayo mgonjwa hutakiwa kunywa maji ili sehemu ya tumbo na utumbo zipate kuonekana vizuri wakati wa kupima.
    Nb: vipimo hivi havipatikani kirahisi nchini kwetu hivyo madaktari hutumia akili zao ambazo zimefundishwa kutambua ugonjwa huo bila ata vipimo.

    MATIBABU;
    Ugonjwa huu unatibika na kupona kabisa sio kama watu wengi wanavyodai hauponi na kukaa nao miaka huku wakiteseka.
    Mchanganyiko wa dawa kitaalamu kama triple therapy umeonyesha kutibu ugonjwa huu kabisa .{omeprazole, amoxycline,metronidazole} au {lansoprazole, scenidazole, clarithromycin}
    Pia unaweza kutumia mchanganyiko wa cimetidine, amoxyline na metronidazole kulingana na uwezo wa kuzipata dawa hizo
    Dawa za kupunguza tindikali tumboni ni nzuri sana kupunguza dalili na maumivu. Mfano magnesium transilicate tablets.

    Kwanini watu wengi hawaponi ugonjwa huu?
    • dozi ya ugonjwa huu sio chini ya wiki nne, lakini utakuta mtu anameza dawa  kwa wiki moja tu na kuacha au pale anaposikia maumivu tu ndo anameza.
    • kuendelea kunywa pombe na kuvuta sigara wakati ugonjwa bado haujapona.
    • Kula vyakula vya moto sana au baridi sana kipindi cha ugonjwa.
    • Kula nyama kwa wingi kipindi cha matibabu.{ nyama inapoliwa tindikali nyingi hutolewa na nyongo kumeng”enya nyama hiyo{ lakini pia tindikali hiyo ni hatari sana kwa vidonda vya tumbo}
     Matibabu ya asili:
    Utafiti wa chuo kikuu cha stanford umebaini unywaji wa juice ya kabechi mbichi kwa kiwango cha 250mils{ujazo wa kikombe cha chai} kila baada ya masaa sita umeonyesha kutibu kabisa tatizo hili ndani ya wiki mbili tu. 
    MWISHO; dawa yeyote ambayo inaandikwa kwenye makala hizi inatakiwa uitumike kwa kuandikiwa na maelekezo ya daktari hivyo nakushauri uonane na daktari  au utupigie tukuelekeze. kwa maelezo zaidi bofya maneno hayo ya kijani kusoma

    SECRETS OF GOOD HEALTH


                                                   STAY ALIVE

                                    MAWASILIANO 0653095635/0769846183

                                 DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

            




                                      



    KAMA WEWE MWANAUME UNA TATIZO LA KUFIKA KILELENI HARAKA KABLA MPENZI WAKO HAJARIDHIKA SOMA HAPA

                                           
    Pre mature ejaculation ni nini?
    Hii ni hali ambayo mwanaume anatoa mbegu mapema sana kipindi cha tendo la ndoa na mara nyingi huambatana na kushindwa kumridhisha mpenzi wake.



    Tatizo hili limekua likiwapata wanaume wengi na kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa baada  ya hali hii kutokea.
    Kimsingi  mwanaume anatakiwa achukue dakika nne mpaka nane kabla ya kutoa mbegu za kwanza lakini watafiti wanasema tatizo hili hugundukiwa mtu anapotoa mbegu ndani ya dakika moja au kabla ya dakika moja.
    Tatizo hili huweza kutokea mara tu baada ya kubalehe,{primary pre mature ejaculation} mda mrefu baada ya kubalehe{secondary PE} au kutokana na aina ya mwanamke uliompata.{situational PE}

    Chanzo ni nini?
    Tatizo hili halina sababu za kitaalamu zilizofanyiwa utafiti zikakakubalika ila wanasayansi wanaamini sababu zifuatazo zinaweza kua chanzo kikuu cha tatizo hilo.

    kupiga punyeto au kujichua; mara nyingi watu wanaopiga punyeto hua wanafanya haraka kwa kujificha ili wasikutwe na mtu. tabia hii ya kulazimisha mbegu zitoke haraka huweza kuleta tatizo hili kwa kubadilisha mfumo wa mwili unavyofanya kazi.

    kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa; kukaa mda mrefu sana bila kushiriki tendo la ndoa husababisha mkusanyiko mkubwa wa mbegu za kiume ambazo zinaleta msisimko mkubwa na matokeo yake ni sekunde chache tu umeshaharibu. kawaida mwanaume anatakiwa ashiriki tendo angalau mara tatu kwa wiki.

    kuwa na wasiwasi wakati wa tendo la ndoa; mtu akiwa na historia ya kupata  hali hii kabla, hua hajiamini na kua na wasiwasi kwamba litatokea tena na matokeo yake hulipata kweli.

    madhara ya dawa zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu; baadhi ya dawa za usingizi, mawazo na zingine zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu huleta tatizo hili mfano amitriptyline.

    kurithi; baadhi ya koo au familia fulani hurithi vimelea vya kua na ugonjwa huu kwa vizazi mbalimbali vya familia husika.

    magonjwa ya mfumo wa uzazi wa mwanaume mfano prostatitis.


    Diagnosis{ kuutambua ugonjwa]
    Mwanaume yeyote ambaye anatoa mbegu chini ya dakika moja au mbili ni muhanga wa hili tatizo na anatakiwa apewe matibabu.
       

    Matibabu
    Matibabu ya ugonjwa huu yamegawanyika sehemu kuu mbili kulingana na ukali wa tatizo husika.

    ·         Non pharmacological treatment{matibabu yasiyo hitaji dawa}:  matibabu haya hupewa watu ambao wanahimili mpaka dakika tatu bila kutoa mbegu.

    ·         Pharmacological treatment{matibabu yanayohusu dawa}: matibabu haya hupewa watu ambao hutoa mbegu ndani ya dakika moja baada ya kuanza kushiriki tendo la ndoa, watu hawa hushauriwa kutumia na mbinu zote mbili za matibabu.


    Yafuatayo ni matibabu yasiyohitaji dawa.


    ·         Tumia condom:
    Condom ni moja ya tiba nzuri ya tatizo hili kwani hufanya kazi kwa kupunguza hisia kali za mapenzi mtu anazozipata pale ambapo hatumii condom.

    ·         Kandamiza perineum kwa kidole:Perineum ni eneo kati ya mkundu na korodani, ile sehemu ikikandamizwa na kidole huweza kuzuia kukojoa haraka wakati wa tendo la ndoa.
    .
    ·         Punguza wasiwasi: hebu lifikirie tendo hili kama njia ya kujifurahisha sio njia pekee ya kutafuta kumwaga,  hii itakusaidia kuondoa mawazo ya kutafuta kumwaga na kuchelewa kumaliza.

    ·         Fanya taratibu: picha za ngono zinadanganya sana watu kwamba kulala na mwanamke lazima ufanye kwa haraka haraka kama mbwa. HAPANA; ukifanya taratibu ndio njia nzuri ya kumfikisha mwenzako na wewe kuchelewa kufika kileleni.


    ·         Badilisha style: ile style ya zamani ya kumlalia mwanamke kwa juu{missionary position} inaleta msuguano mkubwa kwenye kichwa cha uuume hivyo itakufanya ufike haraka sana.
     Tumia style ya wewe mwanaume kutangulia chini afu mwanamke juu au kulala kwa upande wote mnaangalia upande mmoja hii itakusaidia sana kuchelewa


    ·         Toa mawazo kwamba unafanya ngono: hebu jaribu kufikiria mambo mengine ya kikazi au masomo wakati unafanya tendo hilo, hii itakupunguzia hisia kali za mapenzi na kuchelewa kufika.


    ·         Fanya na kuacha: hii ni ile hali ya kuzuia msuguano pale unapoona unakaribia kutoa mbegu kwa kama sekundi 30 kisha unaanza upya. Hakikisha haufiki “point of no return”. pointi ambayo huwezi kujizuia tena kumaliza.

    ·         Kandamiza sehemu ya shingo la uume: hii sehemu ya shingo ya uume kwa chini ambayo ukiibana itakusaidia kuanza upya tena kihisia. Nimetumia shingo la uume kwasababu najua uume hauna mabega.

    tumia kilevi: unywaji wa pombe mfano bia mbili kwa siku kwa wanaume pombe hupunguza kidogo nguvu ya mishipa ya fahamu na kufanya mtu aliyekunywa kuchelewa sana kufika kileleni, [watu wanaokunywa pombe lazima mtakubaliana na hili] hivyo unaweza kunywa bia, wine au whisky nusu saa kabla ya tendo na kuondoa shida hii.

    ·      
    Matibabu ya kutumia dawa.
    hizi hupewa iwapo tatizo lako ni kubwa sana na hizo njia hapo juu zimeshindikana...
    1.       Serotonin reuptake inhibitors mfano paroxetine na  clomipramine zimefanya kazi nzuri ya kuzuia kufika kileleni haraka..... humezwa saa moja kabla ya tendo la ndoa.

    2.       anesthetic creams:  hii hupakwa kwenye kichwa cha uume saa moja kabla ya tendo la ndoa kuzuia msisimuko na kufanya mwanaume achelewe kufika kileleni wakati wa tendo.[dawa hizi hazipatikani ndani ya nchi hivyo tunaagiza nje kama ukihitaji wasiliana nasi kwa namba hapo chini]

    h                   
                                        mawasiliano...  0769846183/0653095635

                                   DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                      

                                                          STAY ALIVE...





           

    MATATIZO YA KUKOSA USINGIZI {INSOMNIA}


                                                                                
                    

    Insomnia ni nini?

    Huu ni ugonjwa ni ugonjwa ambao huambatana na tabia zifuatazo..

    • ·         Kushindwa kupata usingizi kabisa.

    • ·         Kulala na usingizi kuisha usiku sana na kushindwa kulala tena.

    • ·         Kubadilika kwa mfumo wa kulala I:e  mtu wa aina hii husinzia mchana na kukosa usingizi usiku.

    • ·         Kusinzia haraka baada ya kufika kitandani  na usingizi kuisha haraka kisha kushindwa kupata usingizi tena.


    Ugonjwa huu husababishwa na nini?
    • ·         Utumiaji wa madawa kama cocaine, nicotine,cafaine na unywaji wa pombe uliopitiliza.

    • ·         Magonjwa ya moyo ambayo humfanya mtu ashindwe kupumua vizuri wakati wa kulala.


    • ·         Maumivu makali ya mwili kama kidonda, kuvunjika mfupa, misuli na kadhalika.

    • ·         Matatizo ya mfumo wa chakula kama kiungulia na kupata choo ngumu.


    • ·         Mazingira mabaya ya kulala kama kelele nyingi na harufu kali.

    • ·         Msongo mzito wa mawazo



    • ·         Utumiaji wa ovyo wa dawa za kuleta usingizi mfano diazepam maarufu kama valiam.


    • ·         Upungufu au ongezeko la homoni za uzazi hasa kipindi cha uzeeni kwa wanawake{menopause} .

    MATIBABU
    Matibabu ya ugonjwa huu yamegawanyka katika sehemu kuu mbili kama ifuatavyo.

    Matibabu yasiyotumia dawa{non pharmacological treatment}:

    kikubwa kinachofanyika hapa ni kuacha tabia zote ambazo ziko ndani ya uwezo wako ambazo zinakufanya ukose usingizi kama nilivyozianisha hapo juu. Aina hii ya matibabu ni nzuri na bora zaidi kuliko matumizi ya dawa za kuleta usingizi ambazo mara nyingi zinasababisha kuzitegemea yaani bila hizo haulali{dependence} na kuleta madhara mengine ya kiafya.
    • ·         Usile chakula kingi wakati wa kwenda kulala.
    • ·         Usinywe kahawa wakati wa kwenda kulala
    • ·         Kitanda kitumike kama sehemu ya kulala sio kuangalizia video na kucheza game.
    • ·         Usiangalie video za kutisha wakati wa kwenda kulala.
    Matibabu ya dawa {Pharmacological treatment}
     
    Magonjwa yanayosababisha{underlying causes} mtu kushindwa kulala yanatakiwa yatibiwe kwanza.  mfano maumivu makali  ya mwili kutokana na magonjwa flani.
    Baadhi ya dawa hutumika kwa mda mfupi kutibu ugonjwa huu kwa  kupunguza dalili kali za mwanzo kisha matibabu ya bila dawa huendelea.

    Dawa hizo ni kama zifuatazo.
    • ·         Antidepressant mfano amitripyline.

    • ·         Benzodiapines mfano diazepam

    • ·         Opiods mfano morphine pale mgonjwa anapokua na maumivu makali sana.

    Kuna dawa nyingi sana zinazotumika ila hizo ni baadhi tu na ambazo zinapatikana kwenye nchi yetu kirahisi.

                   note; only true inner peace of mind can gurantee a good night sleep..

                                     tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

             
             

              
                                                  STAY ALIVE..... 

                                DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
     
                                      0653095635/0769846183



    KAMA WEWE NI MMOJA YA BAADHI YA WANAUME WANAOTAFUTA DAWA YA KUONGEZA MAUMBILE YAO YA KIUME SOMA HAPA ..


                                                                

    utangulizi
    Kwa miaka mingi wanaume wengi wamekua wakijihisi wana nyeti ndogo kulingana  hadithi wanazosikia mtaani kuhusu wanaume wengine wenye maumbile makubwa, video za phonograph,na tabia za kuoga pamoja hasa shule za bweni kipindi cha masomo ya sekondari.
    Kampuni zizodai zinaweza kuongeza maumbile ya kiume zimetengeneza pesa nyingi sana kwa kudai zina vidonge, sindano, na  dawa za asili kwa ajili ya kazi hii.
    Uchunguzi wa kisayansi uliofanyika india umegundua zaidi ya 60% ya wanaume wana wasiwasi na maumbile ya nyeti zao.
    Leo naomba nikutoe dukuduku la  mawazo yako wewe msomaji wa kiume ambaye na wewe unadhani una maumbile madogo na unatafuta suluhisho.
      
    Je ni kweli una maumbile madogo?
    Jibu ni hapana, kwani ukijiangalia mwenyewe  angle unayotumia kujiangalia inakufanya ujihisi una maumbile madogo, lakini mwanaume unayelingana nae maumbile akisimama mbele yako utaona anakuzidi mbali sana kulingana angle uliyosimama kumuangalia yeye.

    Je maumbile ya kawaida yanalinganaje?
    Kosa kubwa linalofanywa na wanaume ni kujipima urefu wa maumbile yao wakati yakiwa yamesinyaa.
     lakini naomba nikwambie kipimo halali cha uume ni pale uume unapokua umesimama tu.
    Nyeti mbili zilizosinyaa zinaweza kuonekana zinatofautiana urefu, mfano moja ikawa na sentimita sita na nyingine tisa lakini zikisimama zote zikafika sentimita 15.
    Utafiti umeonyesha mwanaume wa kawaida ana  uume wenye urefu  sentimita 12 mpaka 15 na unene{circumference} wa sentimita 12  akiwa amesimamisha.
     zaidi ya asilimia 95% ya wanaume wamo kwenye hicho kiwango hicho.
     Japokua kuna wanaume wanakua na uume mkubwa kidogo kuliko vipimo nilivotaja hapo juu lakini uume ni sawa na viungo vingine vya binadamu kama mguu na mikono  na haviwezi kua sawa kabisa.
    Lazima kuna watu wana miguu au viganja vya mikono  vikubwa kidogo kuliko wengine.
     Ni 0.6% ya wanaume wanaoupatwa na hali inayoitwa kitaalamu kama micro penis ambayo uume husimama kwa sentimita saba tu.
    Hali hii husababishwa mara nyingi na kuepo kwa kiwango kidogo sana cha hormone inayoitwa  growth hormone kipindi cha ukuaji.
    Hali huweza kutibiwa na wataalamu wa nyeti{urologist}  bila madhara yeyote.


    Mahusiano kati ya tendo la ndoa na ukubwa wa maumbile ya kiume.
    Utafiti uliofanyika na mtafiti wa kimarekani kwa jina la jonson uligundua wanawake wengi hua swala la ukubwa au udogo wa maumbile halipo vichwani mwao na sio kesi kubwa kama wanaume wengi wanavyolichukulia.
    Swala la kumridhisha mwanamke halina mahusiano na urefu wa uume japokua baadhi ya wanawake walikiri kuridhishwa kirahisi na wanaume wenye uume mnene na sio mrefu kama watu wengi wanavyofikiria.
    Lakini point yangu hapo juu haimaanishi wanaume wenye uume mwembamba hawawezi kuwaridhisha wanawake. La hasha.
    Lakini pia naomba nikuonye wewe mwanamke unayesoma hapa usije ukamwambia mpenzi wako ana maumbile madogo ata kama unatania.
    Kauli hyo ataichukulia uzito mkubwa na itamuumiza sana kichwa kuliko unavyofikiria.
         
    Je kuna dawa ya kuongeza nyeti za kiume?
     Mpaka sasa hivi, Hakuna dawa yeyote ambayo imethibitishwa kuongeza nyeti za kiume kama makampuni mengi yanavyodai.
    Ni operation  na mazoezi tu ndio yamefanikiwa kuongeza maumbile kwa sentimita tatu mpaka tano na zimekua zikiambatana na madhara makubwa kama kubadilika kwa shape za nyeti, kupungukiwa nguvu za kiume, kuchelewa kupona na maumivu ya mda mrefu hasa kawa oparesheni.{chronic pain}
    hata hivyo mazoezi ya kuongeza uume yameonekana hayana madhara kabisa.
    Zaidi ya 75% ya wanaume waliofanyiwa operation hzo hawakuridhika na matokeo yake hivyo sikushauri na wewe uingie huko labda kama una ugonjwa wa micropenis nilioutaja hapo juu.
    Mwisho nakuomba wewe mwanaume ufahamu kwanzia leo kwamba hayo maumbile yako hayana matatizo yeyote na wewe ni dume la mbegu. bonyeza  hapa kwa usahauri na maelezo zaidi

    SECRETS OF GOOD HEALTH


                                          STAY ALIVE…..

                    MAWASILIANO 0653095635/0769846183
                DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO.

    KAMA HAUTUMII VYAKULA HIVI, NGUVU ZA KIUME UTAZISIKIA REDIONI


    .
                                 
    Nguvu  za kiume ni nini?
    Huu ni uwezo wa mwanaume kuweza kusimamisha uume wake na kuhimili mda mrefu kwenye tendo la ndoa bila kuchoka kirahisi.
    Waswahili wanasema ni “uwezo wa gari kupiga starter lenyewe bila kusukumwa”
    Utafiti unaonyesha kati ya wanaume watatu, mmoja ana tatizo la nguvu za kiume kitu ambacho kinaonekana kitakua  zaidi siku zijazo. 
    kwa fursa hii watu wengi wamejiita waganga na kuuza dawa nyingi za uongo wakidai zinaongeza nguvu za kiume ili kujipatia fedha kitapeli.
    nakushauri wewe msomaji usiangukie kwenye mtego huo.
    Kuna sababu kadhaa ambazo zinasababaisha kupungua kwa nguvu hizo lakini hii sio maada yangu kwa leo ila ntaziongelea session zijazo.
        
    Vifuatavyo ni vyakula ambavyo vinaweza kukurudishia nguvu zako za kiume kwa asilimia mia moja{100%].

    ·         Banana {ndizi mbivu}
    Haya ni matunda ambayo yanapatikana kwa wingi nchini kwetu na kwa bei nzuri,  enzyme muhimu iliopo kwenye ndizi kwa jina la kitaalamu  bromelain huongeza stamina na hamu ya tendo la ndoa.
    Pia vitamin B, ambayo hupatikana kwenye tunda hilo huongeza nguvu za mwili.
     
    ·         Garlic {kitunguu swaumu}:
    Kitunguu hichi ni hutumika sana kwenye mapishi ya kiafrika hasa upikaji wa pilau, lakini hufanya kazi vizuri kikiliwa kibichi.
    Kitunguu hichi hufanya kazi ya kuongeza mmiminiko wa damu kwa wingi kwenye uume na kufanya mwanaume kustahimili vizuri kwenye tendo hilo.

    ·         Pea nut{karanga}:
    Karanga ni moja ya vyanzo vikubwa vya amino acid ambayo kitaalamu inaitwa L-arginine ambayo hufanya kazi ya kulegeza mishipa ya damu ya uume na kuruhusu damu kuingia kwa wingi hivyo kuupa uume nguvu maradufu.

    ·         Chocolate:
    Ni chakula kinachopatikana kwa wingi madukani, ambacho kitaalamu kina kemikali zinazoitwa phenylethylamine na alkaloid, ambazo huongeza nguvu na stamina wakati wa tendo la ndoa.

    ·         Blue berries:
    Haya ni aina ya matunda ambayo hayapatikani kirahisi nchini kwetu ila yanalimwa san amerika ya kaskazini na hupatikana mara chache mijini kwenye supermarket kubwa kubwa. Matunda haya hufanya kazi kwa kupunguza lehemu{cholesterol} kwenye mishipa ya damu na kufanya damu kupita kwa wingi kwenye mishipa hiyo na kuufanya uume usimame kwa nguvu na kwa mda mrefu.

        MWISHO: ni kiasi kidogo tu kinahitajika kwa siku, kwa vyakula nilivyotaja hapo juu.
     hivyo sio busara kula vyakula hivyo kwa wingi na kuacha kwa wiki moja.
    Ni vizuri ukala kiasi kidogo kwa mda mrefu ili upate matokeo mazuri.kwa maelezo zaidi soma hapa.


                                                        STAY ALIVE….
                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                            MAWASILIANO 065305635/0769846183